Tumaini katika Kristo (The Hope in Christ) ni huduma ya kiinjili ambayo inahusika na uinjilishaji wa neno la Mungu kwa njia ya mitandao.Huduma hii haifungamani na dhehebu lolote ila inamhubiri na kumtangaza Yesu Krito alie hai.
Tumaini Kichila ndiye muasisi wa huduma hii ambayo aliiasisi nwaka 2015 akiwa na maono ya kupeleka injili kwa njia ya mtandao kwa watu wote haswa ikizingatia ya kwamba wakati huu na dunia ya sasa ni dunia ya mitandao, na mitandao ndio imekua nyenzo kubwa na ya haraka ya kupeleka habari.
Kwa kuwa kizazi cha sasa hivi nikizazi ambacho kinafanya mambo mengi kwenye mitandao, nasi kama Tumaini katika Kristo tukaona ni vyema tukatumia mitandao mbalimbali kupeleka injili kwa watu wote kama neno la Mungu linavyosema katika Marko 16: 15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe”
Kwenye mtandao wetu huu, tutakua na na majukwa mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Jukwaa la kutafakari neno la Mungu – Hapa kutakua na mada kadhaa zitakua zinatolewa na watu kuchangia au kuuliza maswali
2. Kutoka madhabahuni – Hapa tutapata taarifa mbalimbali toka kwenye madhabahu mbalimbali
3. Watoto wetu- Hapa tutapata taarifa mbalimbali za watoto ikiwa ni pamoja na habari toka shule ya jumapili
4. Neno la Leo – Hapa kila siku kutakua na neno fupi na tafakari toka kwa watumishi mbalimbali wa Mungu
5. Afya yetu – Hapa tutapata taarifa mbalimbali zinazohusu afya toka kwa wataalam wa afya
6. Kutana na Mtumishi wako – Hapa utapata nafasi ya kukutana na watumishi mbalimbali wa Mungu na kujua huduma zao au kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu
7. Ndoa zetu – hapa utapata taarifa zinazohusu ndoa ikiwa ni pamoja na sherehe za harusi, send off n.k.
Karibu sana na uwe huru kuleta habari yoyote inayomhusu Yesu Kristo
Hello this is test